Washitakiwa watano kesi ya mauaji ya Dkt. Mvungi wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

0
36

Washtakiwa namba 1, 2, 3, 4 na 6 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya Dkt. Sengondo Edmund Mvungi.

Hukumu hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam ambapo pia mahakama imemuachia huru mshitakiwa namba 5 katika kesi hiyo.

Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi vielelezo vilivyowasilishwa na jamhuri isipokuwa kwa mshitakiwa wa tano ambaye imeona ushiriki wake haukuthibitishwa ipasavyo pasipo kuacha shaka.

Dkt. Mvungi ambaye alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alivamiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Novemba 3, 2013 na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.

Send this to a friend