Washtakiwa wa mauaji ya Askari Loliondo waachiwa huru

0
41

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru washtakiwa wote 24 wa kesi ya mauaji ya Askari wa Jeshi la Polisi, Koplo Ganus Mwita, yaliyotokea Juni 10, 2022 wakati wa zoezi la uwekaji wa mipaka katika pori Tengefu katika Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Washtakiwa hao wakiwemo wananchi na viongozi wanachi wa Tarafa ya Loliondo wameachiwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

CHADEMA yatishia kutoshiriki uchaguzi mkuu 2025

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Juni 16 mwaka huu mbele ya Hakimu Herieth Mhenga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kupanga njama za mauaji kwa maafisa wa polisi pamoja na kusababisha kifo cha Askari Polisi.

Awali, kesi hiyo ilikuwa na watuhumiwa 27 baadaye Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) aliwaachilia watuhumiwa watatu na kusalia watuhumiwa 24 ambao nao wameachiwa wote mahakamani hapo.

Send this to a friend