Wasichana 604 waliorudishwa shuleni waacha tena

0
37

Wasichana 604 kati ya 3,333 wenye umri wa miaka 13 na 21 waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali na kupewa fursa ya kurejea shuleni kupitia mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP- AEP) wameacha tena masomo yao.

Akizungumza mratibu wa mradi wa SEQUIP kitaifa wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Baraka Kionywaki wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa walimu 75 wa masomo ya Sanaa kutoka mikoa 14 mjini Morogoro, amesema wanafunzi hao walisajiliwa katika mwaka wa masomo 2022 katika vituo 168 nchini.

Bajaji zasababisha mgomo wa daladala Arusha

Aidha, amesema baada ya kuona changamoto hiyo, taasisi kupitia mradi huo ulifanya utafiti ili kubaini kinachosababisha wanafunzi kukatisha masomo licha ya kupewa fursa na Rais Samia Suluhu na kubaini kuwepo kwa changamoto ya hali ya kiuchumi kwa wazazi ambapo wasichana hao hulazimika kufanya kazi za ndani ili kujipatia kipato.

Ameongeza kuwa utafiti huo umegundua kuwa wanafunzi wengine wameshindwa kuhudhuria masomo yao kutokana na kukosa watu wa kuwalelea watoto wao pindi wanapokuwa shuleni, hivyo kukatisha masomo yao.

Send this to a friend