Wasifu wa Marehemu William Ole Nasha (1972-2021)

0
24

Aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Mbunge wa Ngorongoro (CCM), William Tate Ole Nasha alifariki dunia jijini Dodoma Septemba 27 mwaka huu.

Ole Nasha alizaliwa Mei 27, 1972. Alihitimu elimu ya msingi mwaka 1984 katika Shule ya Msingi Kakesio, kisha akajiunga Arusha Catholic Seminary Secondary School kwa elimu ya upili ambayo alihitimu mwaka 1989.

Aliendelea na elimu ya kidato cha tano na sita shuleni hapo na kuhitimu mwaka 1992.

Mwaka 1996 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisoma Shahada ya Awali ya Sheria na kuhitimu mwaka 1999.

Kati ya mwaka 200 na 2001, Ole Nasha alisoma Shahada ya Umahiri ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini.

Alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro kwa mara ya kwanza mwaka 2015, na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli akamteua kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Mwaka 2017 alihamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika ngazi hiyo hiyo ya Naibu Waziri, nafasi aliyoishika hadi Oktoba 2020.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020, Ole Nasha alichaguliwa tena kuwa mbunge wa jimbo hilo, na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Uwekezaji iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 2019.

Mwili wa mwendazake William Tate Ole Nasha utazikwa Jumamosi, Oktoba 2,mwaka huu kujijini kwao mkoani Arusha.

Send this to a friend