Wasifu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania
Hisham Hendi alizaliwa mwaka 1980 nchini Misri, kwa sasa anafanya kazi na kuishi nchini Tanzania. Hendi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania Plc.
Hisham alizaliwa na kukulia jijini Cairo ambapo alipata elimu yake ya awali kutoka Manor House International School kati ya mwaka 1986 hadi mwaka 1997.
Alitunukiwa Shahada ya Awali katika Usimamizi wa Biashara (Business Management), kutoka Idara ya Biashara, Chuo Kikuu cha Cairo nchini humo.
Mbali na shahada hiyo pia amehitimu programu mbili za kiutendaji (executive programs) kutoka Shule ya Biashara IMD (IMD Business School) nchini Uswisi na Shule ya Biashara ya London (London Business School) nchini Uingereza.
Hisham ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc akiwa na jukumu la kuendesha shughuli zote za kibiashara, ambapo ana uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika sekta ya mawasiliano ya simu.
Kabla ya kukalia wadhifa huo, Hashim alisimamia mapinduzi makubwa katika idara ya biashara, ambapo alianzishia njia mbalimbali za utofauti za kuwahudumia wateja.
Shauku yake kubwa ya maendeleo ya kidijitali, na uzoefu wake mkubwa katika kuhudumia wateja, ulijihirisha kwa kuanzishwa programu mbalimbali kama Tuzo Points, kadi za kimtandao za M-Pesa, ‘Google play carrier integration, device financing program na un-limited access to digital content’ ambazo kwa pamoja zimeiwezesha Vodacom Tanzania Plc kuendelea kuongoza katika soko, dhidi ya wapinzania wake.
Kabla ya kuja nchini Tanzania, Hashim alifanya kazi kama Mkuu wa Idara ya Bishara wa Vodacom International Business, yenye makao yake nchini Afrika Kusini, ambapo aliongoza utengenezaji na utekelezaji wa mikakati yote ya kibiashara katika masoko yote ya Vodacom barani Afrika.
Pia amewahi kuwa mjumbe wa bodi ya Vodacom Tanzania na Vodacom Msumbiji.
Kabla ya hapo amewahi pia kufanya kazi Vodafone Group London, ambapo alijikita katika kushughulikia masoko katika nchi 13 tofauti kutoka Latin America, Ulaya na Mashariki ya Kati. Pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu katika kampuni ya Vodacom nchini Misri, ambapo alikuwa akishughulikia digitali na maudhui, malipo ya kabla na baada pamoja na shughuli za masoko ya wateja.
Hisham aliitumikia AIESEC kwa miaka mine, ambapo alikuwa rais wa taasisi hiyo nchini Misri 2000-2001, alidhaminiwa na Procter & Gamble International, na alitunukiwa tuzo ya ‘best local committee performance in Africa mwaka 2001.’
Hisham alioa mwaka 2007, yeye na mkewe Dalia Nadim wana watoto wawili, Lana Hendi na Adam Hendi, na wote wanaishi Tanzania.
Hisham ni muumini mkubwa wa masuala ya dijitali pamoja na fursa zake katika kubadili na kuboresha maisha.
Amewahi kuonekana katika majukwaa mbalimbali kama vile GSMA na PMI akizungumza juu ya mabadiliko ya kidijitali, pamoja na nafsi ya teknolojia ya simu katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi katika jamii.
Pia, amewahi kuhojiwa na gazeti la The Citizen akielezea namna teknolojia inaweza kutumika kufanikisha mabadiliko chanya katika jamii.