Wasiochanjwa kuzuiwa kuingia kwenye ofisi za serikali

0
47

 

Serikali ya Misri imetangaza kuwa kuanzia katikati ya mwezi ujao itawazuia watumishi wa umma ambao hawajachanjwa kuingia katika majengo/ofisi ya serikali.

Taarifa ya baraza la mawaziri iliyotolewa Oktoba 17 mwaka huu imesema watumishi hao watatakiwa kuchanjwa ama kupima Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) kila wiki ili kuruhusiwa kuingia kwenye ofisi hizo kuanzia Novemba 15.

Baraza hilo pia limeruhusu kufunguliwa kwa maliwato kwenye misikiti kuanzia Jumatano ambayo yalikuwa yamefungwa kuanzia Machi mwaka jana ikiwa ni sehemu ya njia za kukabiliana na UVIKO19.

Hadi sasa Taifa hilo limetoa zaidi ya dozi milioni 30 za chanjo kati ya raia wake ambao ni zaidi ya milioni 100, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya nchini humo.

Send this to a friend