Msemaji wa Bunge la Uganda amewakosoa vikali watu wasiojulikana ambao wamehariri taarifa za Spika wa Bunge kwenye ukurasa wa Wikipedia na kuonesha kwamba amefariki dunia.
Chris Obore amesema kuwa hali ya afya ya kiongozi huyo itaelezwa na msaidizi wake, Naibu Spika, ambaye amekwenda nchini Marekani ambako Spika Jacob Oulanyah anaopatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.
Kumekuwa na hisia tofauti kutokana na safari zake nje ya nchi kupata matibabu, ambapo wakosoaji wamesema kwamba inagharimu fedha nyingi za walipakodi.
Obore amesema waliobadili taarifa za spika walitumia uficho ‘virtual private network’ hivyo hawajapatikana.
Wikipedia hutoa fursa kwa mtu yeyote kuhariri taarifa mbalimbali, lakini kuna baadhi ya wasimamizi ambao hutunza baadhi ya kurasa zisihaririwe hovyo.