Wasira: Kaulimbiu ya No Reforms, No Election inakwenda kufikia mwisho

0
6

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesisitiza kuwa hakuna mtu au kikundi cha kuzuia uchaguzi huku akiwataka wananchi kutobabaishwa na kaulimbiu ya ‘No Reforms, No Election’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa inakwenda kufikia mwisho.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa katika kikao cha ndani wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma ambapo amesema baada ya Rais Samia Suluhu kuingia madarakani aliamua kuja na mfumo wa maridhiano na kupitia maridhiano kuna mambo mengi ya msingi yamefanyika.

“Usibabaishwe na maneno hakuna mtu wa kuzuia uchaguzi, utakuwepo na ninyi mabalozi toeni watu wetu waende wakapige kura muda ukifika, waende wakatiki na tiki yenyewe ni rahisi maana unaona CCM na alama ya jembe na nyundo,” amesema Wasira.

Ameongeza, “Hii kaulimbiu ya ‘No Rerfoms, No Election’ isiwazuie kulima korosho, isiwazuie kupiga ‘selfie’. Hamna kitu hapa ninyi endeleeni kwenda kujiandikisha, narudia hii kaulimbiu mwisho wake unakaribia.”

Aidha, Wasira amewahakikishia wananchi kuwa nchi iko salama huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza kuwa Tanzania hakuna kubaguana kwa dini, rangi wala kabila.