Aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Bunda, Stephen Wasira, ameshauri viongozi wa dini kutojihusisha na siasa badala yake kuhubiri amani ili kuepusha mivutano ya kisiasa kwa waumini na kuleta umoja.
Ameyasema hayo wakati akichangia kwenye mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini na wadau wa Demokrasia katika ukumbi wa Kimataifa JNICC, mkutano ulioanza Septemba 11, 2023.
“Tulishakubaliana, kila mtu ana dini yake na tunaheshimu viongozi wetu wa kiroho, na tena nawashauri, tunazungumzia amani. Baba Askofu, unaendesha watu katika kanisa ambalo lina vyama vyote, ukiwaambia waumini wako wewe ni CCM na wewe unaleta tatizo kwenye kanisa, maana watagombana wa CHADEMA kanisani, chama chako kaa nacho tu kimya kimya.
Cleopa Msuya: Tusijisahau tukaelekea kwenye machafuko ya siasa
Lakini usiwalazimishe wakufuate, tukifanya hivyo tunapa shida, tunaigawa nchi yetu, tunaleta hisia zinazokosesha nchi amani, ambayo ni msingi wa yote haya,” amesema.
Aidha, amesema uraia wa nchi hii ni mmoja pekee na hakuna nchi inayoitwa Zanzibar wala Tanganyika, hivyo Watanzania kwa ujumla waendeleze umoja huo ulioanzishwa na waasisi wa taifa.