Wasusia mazishi wakidai marehemu hakushiriki shughuli za kijiji

0
50

Katika hali ya kushangaza kanisa moja huko Kisii nchini Kenya, limelazimika kuingilia kati na kufanya mazishi ya mwanaume mmoja ambaye mwili wake ulikaa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa muda wa wiki tatu kutokana na wakazi wa eneo hilo kususia msiba huo.

Hiyo ni baada ya wakazi wa eneo hilo katika kijiji cha Mokongonyoni kudai kuwa marehemu Linet Kerubo (33) hakuwa na mchango wowote katika shughuli zilizofanyika kijijini hapo pindi alipokuwa hai hasa katika misiba.

Inaelezwa kuwa, Kerubo alikuwa akiishi na mama yake, Elmelda Otora ambaye amekuwa akishiriki na kujitoa kwa kiasi kikubwa katika mambo mbalimbali yanayotokea katika eneo hilo, haswa yale yanayohusiana na vifo.

Mnada wa kuuza vitu vya Mandela nchini Marekani umesitishwa

Hata hivyo, wakazi hao wanadai kuwa marehemu alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 18 na alipaswa kuchangia kikamilifu masuala ya kijiji na haijalishi mchango wa mzazi wake.

Kwa mujibu wa ripoti za ndani, baada ya wakazi hao kuona kwamba kanisa limeingia kati kushughulikia suala hilo, walitaka kushiriki kwenye mazishi hayo lakini kanisa lilikataa ombi lao na kusema kuwa “waliiacha familia hii ilipowahitaji zaidi.”