Wataalam: Usikae zaidi ya dakika 10 maliwatoni ni hatari kwa afya

0
47

Inaweza kuonekana kama jambo la kawaida na lisilo na madhara kutumia muda mrefu unapokuwa maliwatoni. Hata hivyo, wataalamu wanaonya kuwa kukaa muda mrefu chooni kunaweza kuathiri afya yako.

Kulingana na Dkt. Lai Xue, daktari bingwa wa upasuaji wa utumbo mpana katika Chuo Kikuu cha Texas Southwestern huko Dallas, tabia hiyo imehusishwa na hatari ya kupata bawasiri na kudhoofika kwa misuli ya nyonga.

Dkt. Lai anasema kukaa muda mrefu maliwatoni kunaweza kuhatarisha afya kwa sababu husababisha mgandamizo kwenye sehemu ya chini ya mwili, hali inayosababisha mzunguko wa damu kuzorota. Hii husababisha mishipa ya damu kuvimba, jambo ambalo linaweza kuongeza hatari ya kupata bawasiri na kudhoofisha misuli ya nyonga.

Watu wanapaswa kutumia wastani wa dakika tano hadi kumi maliwatoni, kulingana na Dkt. Farah Monzur, profesa msaidizi wa tiba na mkurugenzi wa Kituo cha Magonjwa ya Matumbo katika Stony Brook Medicine huko Long Island, New York.

Aidha, Dkt. Monzur anasema watu wanaotumia muda mrefu wakiperuzi simu zao wakiwa maliwatoni, hujikuta wakikaa muda mrefu bila kujitambua, na kuwafanya wajikaze zaidi kutoa kinyesi, hali inayochangia kuongezeka kwa shinikizo ambalo linaweza kusababisha bawasiri

Send this to a friend