Wataalam waeleza sababu kuu 3 za wanaume kukosa nguvu za kiume

0
52

Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam, Dkt. Elisha Osati amesema kuna vitu vingi vinavyoweza kuathiri nguvu za kiume ikiwemo sababu za maumbile, hali ya lishe pamoja na hali ya kisaikolojia.

“Kuna watu wameumbwa miili yao haiwezi kutengeneza homoni za kiume kwa wingi. Kuna mambo yanapunguza uzalishaji wa homoni kama magonjwa sugu kama kisukari, uzito kupindukia na kutofanya mazoezi,” amesema.

Daktari ameeleza kuwa kuna wakati tatizo hilo linakuwa la kisaikolojia zaidi na kwamba kila mwanaume katika maisha yake aliwahi kushindwa kusimamisha uume kwa sababu moja au nyingine.

Mambo 10 unayoweza kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani

Aidha, Daktari Bingwa wa magonjwa ya binadamu, Dkt. Boaz Mkumbo amesema baadhi ya wanaume wenye umri chini ya miaka 35 wamejiathiri kisaikolojia kwa kujichua, kutumia dawa za kemikali za kuongeza hisia na kulazimisha kuunganisha tendo la ndoa bila kupumzika baada ya kufika kileleni.

“Wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka miaka 35 wengi wao unakuta wameathirika na maradhi kama kitambi, kisukari, shinikizo la damu, mwili kuwa katika wingi wa sumu za vyakula, kunywa pombe kupindukia, uvutaji sigara na dawa za kulevya, magonjwa yatokanayo na lishe pamoja na magonjwa ya homoni ambayo hupunguza hisia kwa kasi sana,” ameeleza.