Wataalamu: Wimbo wa Taifa unakosewa namna ya kuimbwa

0
39

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu leo Mei 10, 2022 jijini Dodoma amekutana na wataalamu wa ala za muziki wakiongozwa na Mwalimu Mstaafu wa Shule za Sekondari Alexander Ngonyani ambao wanapitia Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo na Wimbo wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika wakati wa uimbaji na hatimaye kuyarekebisha ili nyimbo hizo ziimbwe kwa usahihi.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Yakubu amesema kuwa Wimbo wa Taifa ni miongoni mwa Tunu za Taifa, hivyo unapaswa kuheshimiwa.

“Nawasisitiza kubainisha makosa yaliyopo kwenye nyimbo hizo, pamoja na usahihi unaotakiwa ili sisi kama Serikali tuchukue hatua ikiwemo kutoa elimu Kwa jamii ili makosa hayo yasirudiwe”Amesema Bw.Yakubu.

Kwa upande wake Mzee Ngonyani amesema kuwa chimbuko la kazi hiyo ni kutokana na kubaini makosa mengi katika uimbaji wa nyimbo hizo unaofanywa na taasisi, shule na katika hafla mbalimbali za kitaifa, na tayari ameshawasiliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na BASATA ambao wamepokea utafiti huo ambao na kushauri aonane na uongozi wa Wizara ili kufanyiwa kazi ipasavyo.

Send this to a friend