Watafiti wabaini kupungua kwa manii kwa wanaume

0
19

Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, idadi ya mbegu za kiume za binadamu imeonekana kupungua kwa zaidi ya asilimia 50 kote ulimwenguni, kulingana na tafiti iliyofanywa.

Watafiti wanasema ikiwa matokeo yatathibitishwa na kupungua kukiendelea, inaweza kuwa na athari kubwa kwa uzazi wa binadamu. Wataalam wanasema itakuwa pia kielelezo cha kuzorota kwa afya ya wanaume kwa ujumla.

Mapitio hayo yamezua mjadala kati ya wataalam wa uzazi wa kiume. Wengine wanasema matokeo ni ya kweli lakini wengine wanasema hawajashawishika na data hizo kwa sababu mbinu za kuhesabu manii (sperm) zimebadilika sana kwa muda na kwamba haiwezekani kulinganisha namba za zamani  na za kisasa.

Namna 5 ya kuepuka kupatwa na kiharusi

“Kuna uhusiano mkubwa kati ya afya ya uzazi ya mwanamume na afya yake kwa ujumla. Labda hatuna afya kama tulivyokuwa zamani, “amesema Dkt. Michael Eisenberg, daktari wa urolojia wa Stanford Medicine.

Imeelezwa kuwa katika kiwango cha idadi ya watu, wastani wa idadi ya mbegu za kiume ilipungua kutoka milioni 104 hadi milioni 49 kwa mililita kutoka 1973 hadi 2019. Namba za kawaida za manii zinakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 40 kwa mililita.

Hata hivyo takribani wataalam wote wanakubali kwamba suala hili linahitaji utafiti zaidi.