Watakaojifungulia nyumbani faini TZS 50,000

0
46

Serikali ya Kijiji ya cha Marumba kilichopo wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara imeanza kuwapiga faini ya shilingi 50,000 akina mama wote watakaobainika kujifungulia nyumbani.

Hatua hiyo inalenga kupiga vita mila na desturi ya baadhi ya akina mama hao ambao huamini kujifungulia nyumbani ni ushujaa na inaleta heshima kwa wenzao.

Ashitakiwa kwa kujifanya Rais Samia mtandaoni

Hata hivyo, wataalamu mbalimbali wamekuwa wakishauri wajawazito kujifungulia hospitali ili kuepusha madhara yakiwemo kupoteza damu nyingi, mtoto kupata maambukizi ya kitovu na kujiweka kwenye hatari ya kupoteza maisha kwa kucheleweshwa kupatiwa huduma.

Send this to a friend