Watakaowadanganya mawaziri kuvuliwa nyadhifa zao

0
49

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amesema meneja, mkuu wa taasisi na watendaji wa wizara hiyo wanaotoa majibu ya uongo na kusababisha mawaziri kuonenkana wamelidanganya Bunge, watashughulikiwa.

Akizungumza na mameneja, wakuu wa taasisi na wafanyakazi waliochini ya wizara hiyo mkoani Dodoma Waitara amesema mawaziri wamekuwa wakipokea majibu kutoka kwa watendaji lakini cha kushangaza mara baada ya kuyatoa wanaambiwa wametoa majibu ya uongo.

Amesema kuanzia sasa akipewa jibu la uongo ataomba kibali kwa waziri mkuu kwenda eneo husika na kumvua wadhifa meneja au kiongozi atakayekuwa amehusika kutoa majibu hayo.

Ameeleza kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa wavivu kutekeleza majukumu yao na badala ya kufika eneo la kazi wanafanya kazi kwa simu, hivyo kupelekea kutoa majibu ambayo huenda yamepitwa na wakati au ya uongo.

Send this to a friend