Watano wajitokeza kurekebisha maumbo Muhimbili

0
45

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohammed Janabi amesema hospitali hiyo imepokea watu watano waliojitokeza kujisajili ili kupata huduma ya kurekebisha maumbo inayotarajiwa kuanza Oktoba 27, mwaka huu.

Upasuaji huo ambao awamu hii utafanyika kwa watu sita hadi 10, Prof. Janabi amesema kati ya watu hao, ni mtu mmoja pekee ambaye ameomba kufanyiwa huduma hiyo kwa ajili ya urembo, huku wengine wakiomba kwa ajili ya matibabu.

“Tunategemea wahitaji zaidi, kwa mara ya kwanza hatuwezi kufanya wengi na muda ni mdogo, tutaona kwa sababu tutafanya nyingine na wenzetu wa Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka,” ameeleza.

Waziri aagiza kumbi za starehe, MCs wasajiliwe kabla ya Novemba 30 

Hospitali ya Muhimbili- Mloganzila ilitangaza kuanza zoezi la upasuaji wa kibingwa kwa ajili ya kupunguza uzito na upasuaji shirikishi (Cosmetic Surgery na Bariatric Surgery) ambao utahusisha kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu za mwili kama vile kuongeza matiti, kupunguza mafuta tumboni na kuondoa nyama iliyozidi mwilini.

Send this to a friend