Watano wakamatwa kwa uchochezi mtandaoni dhidi ya viongozi wa serikali

0
38

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo na uchochezi kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Sukununu01 na Jamii Digital, dhidi ya viongozi wa Serikali.

Kamanda wa Polisi, Jumanne Muliro amesema zoezi hilo hilo ni kutokana na ufuatiliaji maalum unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na makosa ya kimtandao.

“Waliokamatwa ni pamoja na Obadia Kwitega (35) mkazi wa Kigamboni na Issa Mwamba (28) mkazi wa Tabata Segerea. Wamekamatwa kwa tuhuma za kumiliki televisheni ya mtandaoni ya kwenye Youtube iliyotambulika kwa jina la Jamii Digital, na akaunti ya mtandao wa X iitwayo Sukununu01, waliyokuwa wanazitumia kusambaza taarifa za uongo na za uchochezi kuhusu viongozi wakuu wa Serikali.

Kamanda Muliro ameeleza kuwa baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye kurasa hizo zilisomeka kuwa “Mkakati wa siri wa January Makamba kumng’oa Rais Samia 2025.”

Send this to a friend