Watano wakamatwa kwa wizi kwenye daladala Mwanza

0
23

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema limewakamata watu watano kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo kwa tuhuma za wizi ndani ya usafiri wa umma (daladala).

Watuhumiwa hao ni Emmanuel Zongoli (42) dereva, Mussa Mkuye (37) kondakta, Mwita Joseph (47) mpiga debe, Shabani Abdallah (47) dereva na Boniphace Mabina (22) kondakta.

Polisi wamesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakati wa operesheni iliyaonza Januari 19, 2026 hadi Januari 31, 2026 kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya uwepo wa vitendo hivyo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Send this to a friend