Watanzania 28 wahukumiwa kwa kuingia Afrika Kusini kinyume cha sheria

0
40

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatiani Watanzania 28 waliokwenda Afrika Kusini kinyume cha sheria ya uhamiaji na kuwaamuru kulipa faini ya TZS 70,000 au kwenda jela miaka miwili.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema watuhumiwa wote wamekiri kutenda kosa hilo ambapo wameiomba mahakama kuwapunguzia adhabu hiyo.

“Kitendo cha kuondoka nchini bila kufuata taratibu siyo kitendo cha busara, wengine mmewatia simanzi familia zetu kwa sababu ndugu zenu walijua mmeshafariki pia mmezitia hasara familia zenu kwa sababu mmerudi bila chochote,” amesema.

Kwa mujibu wa wakili wa Serikali Idara ya Uhamiaji, Shija Sitta amedai watuhumiwa hao walirejeshwa nchini kutoka Afrika Kusini Agosti 20 mwaka huu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kugundulika waliingia nchini humo kinyume cha sheria.

Send this to a friend