Watanzania wafanya maajabu Australia’s Got Talent

0
38

Wanasarakasi wawili kutoka Tanzania, Ibrahim Ramadhani (36) na Fadi Ramadhani (26) wanaojulikana kama ‘The Ramadhani Brothers’ wamewashangaza watazamaji katika kipindi cha Australia’s Got Talent baada ya kufanya onesho la kusisimua.

Majaji walionekana kushtushwa na onesho lao, huku mmoja wa majaji, Kate Ritchie akionekana kuushika uso wake kwa mshangao mkubwa.

“Siwezi hata kuunganisha sentensi kwa sababu sijawahi kuona kitu kama hicho maishani mwangu,” alisikika akiwaambia majaji wenzake.

Katika hali ya kufurahisha baada ya onesho lao la kusisimua, majaji wamewatunuku ‘Golden Buzzer’ ambayo hutolewa mara chache kwa wanaofanya vizuri zaidi hivyo kuingia moja kwa moja kwenye fainali la shindano hilo.

Wawili hao wameeleza matamanio yao kuwa ni kushinda shindano hilo ili kusaidia watoto katika jamii yao pamoja na kuwania rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kupanda ngazi nyingi zaidi huku mmoja akiwa kichwani.

Send this to a friend