Watanzania wanaishi kwa zaidi ya dola moja kwa siku

0
39

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwamba amewakatalia wakuu wa uchumi wa nchi wanaodai kuwa Watanzania wanaishi kwa dola moja kwa siku, na kueleza kwamba  wanaosema hivo wanatumia kipimo cha maisha ya mjini, na sio maisha cha Watanzania wenyewe.

Akihutubia waandishi wa habari mkoani Arusha katika Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani amesema ukiangalia mali au chakula ambacho Watanzania wanaoishi porini wanakula, kwa bei ya nchi za Magharibi ni kubwa zaidi ya dola moja ya Marekani ambayo wanaisema.

“Nikamwambia chukua wale watu wanaokula matunda kule… Huyu ili aishi anakula matunda si chini ya 10 asubuhi, mchana anahitaji mengine lakini jioni kabla ya kulala anahitaji mengine. Nikamwambia hali matunda peke yake, matunda na asali, lakini hivi vitu ni organic [asili]. Nikamwambia sasa twende kwenye supermarket Ulaya tukaangalie bei ya matunda organic, bei ya asali organic ni kiasi gani. Huyu mtu unaniambia anaishi kwa dola moja kwa siku? Sio kweli?” amesema.

Aidha, amewataka waandishi wa habari kuyaandika hayo kupinga upotoshaji unaofanywa na vyombo vya habari vya nchi zilizoendelea ambazo mara nyingi vimekuwa vikiiandika Afrika kama sehemu yenye vurugu, umaskini wa kila namna na mambo mengine hasi, zoezi ambalo wanalifanya kwa kushirikiana na waandishi wa Afrika ambao hujiita mawakala.

Send this to a friend