Watanzania wanaosafiri nje kulipa TZS 40,000 kupimwa Corona

0
41

Serikali imeandaa mwongozo wa kuwapima wasafiri wanaokwenda nje ya nchi hususani zile zenye hitaji la kupimwa maambukizi ya COVID-19 ambapo raia wa Tanzania atalazimika kulipa TZS 40,000 kupata huduma hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya imeeleza kuwa mwongozo huo unalenga kuweka utaratibu wa upimaji wa wasafiri kwa
hiari kwa wanaohitaji kwenda kwenye nchi ambazo zinahitaji wawe wamepima kabla ya safari zao.

Wizara imeelekeza kuwa raia mkaazi wa Tanzania atatakiwa kupa TZS 60,000 huku raia wa Kigeni ikitakiwa kulipa USD100 kupat huduma hiyo.

Utaratibu wa kupima uliowekwa unaelekeza kuwa msafiri atakayehitaji huduma afike katika Hospitali ya Mkoa akiwa na uthibitisho wa uhitaji wa kupima kwa nchi anayotaka kwenda ikiwemo hati ya kusafiria.

Aidha, msafiri anatakiwa kupima siku tano kabla ya siku ya kusafiri kwa sababu cheti cha COVID-19 kitadumu kwa muda wa siku 14 au itategemea masharti ya nchi husika wanapokwenda.

Majibu ya vipimo yatatumwa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa ndani ya saa 72 na kwa wale ambao hawatokuwa na maambukizi watapewa vyeti. Wasafari wote waliopewa vyeti majina yao yatatumwa mipakani kwa ajili ya uhakiki.

Send this to a friend