Watanzania watatu wakamatwa DRC kwa tuhuma za kuwa waasi wa ADF

0
56

Jeshi la  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) limewakamata Watanzania watatu wanaodaiwa kuwa waasi wa kikundi cha Allied Democratic Forces (ADF), waliosajiliwa wilayani Beni, Mashariki mwa nchi hiyo.

Akizungumza Msemaji wa Jeshi, Kapteni Anthony Mwalushay amesema Watanzania hao walikamatwa Februari 6 mwaka huu, wakati wa doria zilizofanywa na sskari wa DRC katika Bonde la Mwalika, eneo la Beni, Kivu Kaskazini. 

Taarifa kutoka FARDC  zinasema, waasi hao wamekiri kuwa wao ni Watanzania ambao waliajiriwa na raia wa DR Congo anayeshi Butembo kwa ajili ya kufanyakazi kwenye mgodi wa dhahabu eneo la Beni, lakini badala yake walijikuta wakiandikishwa kuwa wapiganaji wa ADF. 

“Ni mara ya kwanza kwa Watanzania kukamatwa kwenye nchini humo kwa ajili ya shughuli za waasi za ADF,” ameongeza Mwalushay. 

ADF iliundwa kama muunganisho wa vikundi kadhaa vya waasi, vikiwemo Allied Democratic Movement, the National Army for the Liberation of Uganda (NALU), Uganda Muslim Liberation Army, na wanamgambo wa kundi la Tablighi Jamaat

Send this to a friend