Watanzania wawili wapotea Israel, Serikali yaendelea kuwatafuta

0
36

Serikali imesema kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali nchini Israel inaendelea na juhudi za kuwapata vijana wawili wa Kitanzania wawili ambao hawajulikani walipo mpaka sasa.

Vijana hao ambao ni miongoni mwa vijana 260 waliopo nchini humo kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa hawajaonekana tangu Oktoba 07 mwaka huu kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Israel na tayari familia za vijana hao zimejulishwa.

Korea Kaskazini kufunga ubalozi wake nchini Uganda

Aidha, Watanzania tisa wanaoishi nchini Israel waliitikia wito wa mpango wa Serikali wa kuwarejesha nyumbani na walipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Oktoba 18, 2023.

Send this to a friend