Watanzania wazuiwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na corona

0
57

Raia wawili wa Tanzania wamezuiwa kuingia nchini Kenya kupitia mpaka wa Isibania (mkoani Mara) baada ya vipimo kuonesha wana maambukizi ya virusi vya corona.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mamlaka nchinin Kenya kuweka utaratibu mpya ambao unawalazimu madereva wa malori ya mizigo wanaoingia nchini humo kufanyiwa kwanza vipimo vya COVID-19.

Utaratibu huo mpya umepelekea msongamano mkubwa wa magari mipakani ambapo hadi Mei 12 katika Mpaka wa Namanga kulikuwa na magari zaidi ya 300.

Katika taarifa ya hali ya maambukizi ya virusi vya corona iliyotolewa jana nchini humo, idadi ya visa imepanda na kufikia 715, huku waliopona wakiwa ni 259 na waliofariki wakifikia 36.

Send this to a friend