Watanzania wengi hatarini kuwa vipofu

0
25

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Watanzania wengi wako kwenye hatari ya kupata upofu wa macho kutokana na kutokuwepo huduma za matibabu.

Amesema takwimu zinaonesha kwa mwaka 2021 watu milioni moja pekee ndio waliopata huduma za matibabu ya macho katika vituo vyote vinavyotoa huduma za afya, ilhali waliokuwa wakihitaji huduma hiyo ni watu milioni 12.

“Magonjwa ya macho yanawagusa Watanzania wote, tajiri, maskini wa mjini na vijijini, lakini wanaosumbuka sana ni wale wa kipato cha chini, hivyo ni vema kila mmoja wetu ashiriki kwenye mapambano ya kuzuia magonjwa ya macho,” amesema Waziri Ummy.

Aidha, amewataka wataalamu wa afya kuhakikisha wanatoa elimu juu ya kujikinga na athari ya macho, kwani watu wengi wamekuwa wakiharibu macho yao kupitia simu za mkononi.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend