Ripoti ya utafiti kuhusu mahitaji ya soko la nyumba za kima cha chini Tanzania imeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanajenga makazi ya muda na wengine huchukua mpaka miaka 18 hadi kumaliza.
Utafiti huo umefanywa na kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC) kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya kimataifa ya Habitat for Humanity International (HFHI).
Mkurugenzi wa Huduma za Kifedha za Makazi AHFHI Afrika, Daniel Mhina amesema ripoti imeonyesha Watanzania wa kipato cha chini na cha kati, bado hawana uwezo wa kupata huduma za kifedha kutatua matatizo ya nyumba.
“Zaidi ya asilimia 70 Watanzania wanajenga makazi yao kwa muda na wengine wanachukua mpaka miaka 18 kujenga makazi yao. Unakuta baada ya miaka 18 gharama ya nyumba zinakuwa kubwa sana,” amesema.
Benki Kuu: Pato la Tanzania limekua kwa kiwango cha kuridhisha
Aidha, amesema wamegundua kuna matatizo madogo madogo ya nyumba ambayo Watanzania wanahitaji huku akitolea mfano wa marekebisho ya mabati au madirisha pamoja na kupaka rangi ambapo mtu anapaswa kupata huduma hizo katika taasisi za kifedha lakini changamoto ni kuwa watoa huduma za kifedha hawana mikopo inayoendana na matakwa ya wananchi.
Chanzo: Nipashe