Watatu wafariki baada ya mtumbwi kuzama Ziwa Victoria

0
77

Watu watatu wamefariki dunia na wengine watatu wamenusurika katika kijiji cha Nungwe, wilaya ya Geita mkoani Geita baada ya mtumbwi wao kuzama Ziwa Victoria wakati wakivua samaki usiku wa kuamkia Mei 8, 2023.

Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Geita, Wambura Fidel amesema kutokana na kasi ya maji yaliyokuwa yanaingia kwenye mtumbwi baada ya chombo chao kutoboka yaliwashinda hivyo kupelekea kifo cha wavuvi hao.

Mauaji ya Daktari Tarime: Wananchi walalamikia Jeshi la Polisi

Amewataja waliofariki ni David Maliyatabu (25), Kamuli Mhoja (20) na Faustine Cleophance (28).

Mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Magembe amefika katika eneo la tukio ambapo amewataka wamiliki wa vyombo vya uvuvi kuhakikisha vyombo vyao haviingii majini bila maboya ya kuokolea pamoja na kufanya ukarabati ili kuepuka ajali.

Dickson Alphonce, mmoja wa waliookolewa kwenye ajali hiyo amesema mtumbwi ulipoanza kuingia maji walijirusha kwenye maji kila mmoja kwa lengo la kujiokoa, ndipo watatu kati yao waliokolewa na wavuvvi waliokuwa karibu.

Send this to a friend