Watatu wafariki kwenye mapigano ya wakulima na wafugaji

0
43

Wafugaji wawili na mkulima mmoja wameripotiwa kufariki kwenye mapigano yaliyotokea katika mpaka wa Wilaya ya Nachingwea na Tunduru kutokana na migogoro ya ardhi.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Hassan Moyo amesema vifo hivyo vimetokana na kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wa jamii ya wakulima kutoka katika Kijiji cha Tinginya wilayani Tunduru mkoani Ruvuma waliovamia eneo la malisho la Kijiji cha Matekwe lililotegwa kwa ajili ya wafugaji.

Moyo amewataja waliofariki kuwa ni Nyerere Kisingweda (80), Kidabeleda (31) wote walikuwa wakiishi katika Kijiji cha Matekwe katika eneo lililotengwa kwa ajili ya matumizi ya ufugaji huku mkulima aliyefariki akijulikana kwa jina la Fadhili Nakulamba (32) mkazi wa Kijiji cha Tinginya.

“Nitoe onyo, akiwa kiongozi kama ni wa kisisasa ni mwanaharakati, kiongozi wa dini au kiongozi wa namna yoyote akashawishi watu kuja kuingia Wilaya ya Nachingwea kuja kuvunja amani, kuja kumwaga damu kule, tutamnyofoa sehemu yoyote na tutamshughulikia ili iwe fundisho kwa wemgine wanaojifanya vinara,” amesema.

Aidha, amewataka waliofanya tukio hilo kujisalimisha polisi haraka iwezekanavyo kwa kuwa mkono wa sheria ni mrefu, hivyo kwa namna yoyote watatiwa nguvuni na hatua kali zitachukuliwa kwa wote walioshiriki kupanga njama na kufanya mauaji hayo.

Send this to a friend