Watatu wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua Selemani

0
85

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewahukumu kunyongwa hadi kufa Ahamadi Madi, Juma Malasi na Amiry Miniyama kwa kosa la kumuua Selemani Mohamed mkazi wa kijiji cha Nambau wilaya ya Lindi kwa kumpiga risasi sehemu ya kifuani na kusababisha kifo chake.

Aidha, mahakama imemuachia huru mtuhumiwa namba tatu Salumu Lada baada ya kuonekana hana hatia.

Hukumu hiyo imetolewa Agosti 30, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Lindi chini ya Jaji Rose Ebrahim ambapo watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 16, 2016 huko kijiji cha Nambau baada ya kuwavamia viongozi wa chama cha wakulima AMCOS kwenye kata ya Nyangamala katika kijiji hicho wakati wakiwa ndani ya ofisi wakijiandaa kugawa fedha kwa wanachama wake.

Watuhumiwa hao wakiwa na silaha ya kivita aina ya AK 47 yenye namba 56065529 waliwaweka chini ya ulinzi na kufanikiwa kupora kiasi cha fedha TZS milioni 443.75 kisha kutokomea nazo kabla ya kumpiga risasi kifuani marehemu Selemani Mohamed mpaka Jeshi la Polisi lilipofanikiwa kuwatia nguvuni Januari 07, 2019.

Send this to a friend