Watatu wakamatwa wakijaribu kubadilisha noti bandia benki

0
51

Jeshi la Polisi mkoani Njombe linawashikilia watu watatu Stanley Menda (23), Priva Mbina (23), na Asia Kigoda (24) baada ya kukamatwa na noti bandia 41 za Dola za Marekani zenye thamani ya USD 4100 sawa na TZS milioni 10.3.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Hassan Banga, amethibitisha kukamatwa kwao na kusema kuwa walikamatwa wakati walipokuwa wanajaribu kubadilisha noti hizo katika Benki ya NMB.

“Wamekamatwa na noti 41 za kimarekani ambazo ni bandia, kati ya hizo nne walikuwa wanaenda kubadilisha katika benki ya NMB lakini 37 tumewakamata nazo nyumbani,”amesema.

Aidha, amesema upelelezi zaidi unaendelea kufanyika na mara utakapokamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili kuhusiana na utumiaji wa noti hizo.

Send this to a friend