Watawa wafariki ajalini wakitokea kwenye sherehe

0
44

Watawa watatu wa Shirika la Mtakatifu Benedikto Ndanda mkoani Mtwara wamefariki katika ajali ya gari katika Kijiji cha Mtua Longa Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari walilokuwa wakisafiria (T139 DZZ) kuacha njia na kuanguka kwenye korongo.

Waliofariki ni Padre Comellius Mdoe OSB, Padre Pius Boa OSB na Bruda Bakanja Mkenda OSB ambao walikuwa wakielekea Dar es Salaam kutokea Ndanda kwenye sherehe za nadhiri za daima na za muda.

Aidha, dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo amepata majeraha.

Send this to a friend