Wateja wa betPawa wajishindia TSh53.8 Bilioni ndani ya siku 10

0
40

Dar es Salaam, Novemba 1, 2023…Umekuwa ushindi uliovunja rekodi kwa wateja wa betPawa nchini Tanzania, ambao walijishindia TSh 53.8 Bilioni ndani ya siku 10.Wateja 335,706 tofauti walisherehekea ushindi wakati wa mafanikio ya kuweza kubashiri kwa usahihi kwenye michezo kati ya Jumamosi tarehe 21 na Jumatatu tarehe 30 Oktoba.

Mshindi MKUBWA kuliko wote alijishindia TSh 372.9 Milioni kwa dau la TSh2,200, ikiongezewa na Bonasi ya Ushindi ya 645% kwenye mechi 50 alizobashiri. Hii imedhihirisha kauli mbiu yetu ya betPawa pesa kidogo, ushindi MKUBWA (Bet Small,Win BIG) Kwa jumla wateja 3,738 wa betPawa Tanzania walibadilishwa kuwa mamilionea kwa kipindi cha ndani ya siku 10.

Kutokana na idadi hii kubwa ya washindi ambayo haijawahi kutokea ilisababisha ucheleweshaji wa malipo katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri.Kwetu betPawa kuwa na washindi wengi kumesababisha akaunti zetu za mitandao ya simu kulazimika kuongezwa kiwango cha pesa kila mara kulingana na kiwango cha juu kinachoruhusiwa kwa siku.Hata hivyo tunafanya kazi saa 24 ili kumalizia malipo ya washindi wachache waliosalia.

Meneja wa betPawa nchini Borah Ndanyungu alisema: “Hakuna mtu bora kuliko wateja wa betPawa ambao wameweza kufanikiwa kupata ushindi MKUBWA, na katika kipindi hiki cha

siku 10 wameweza kushinda zaidi kuliko hapo awali.”Aliongeza: “Tunafahamu idadi kubwa ya ushindi umesababisha ucheleweshaji katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri na sisi betPawa tunafurahi kuwa tayari tumeweza kulipa washindi wengi tayari mpaka sasa. Tunafanya kazi bila kuchoka ili washindi wachache waliobakia mwisho walipwe.”

 

: Kwa maelezo zaidi wasiliana na lola.okulo@betpawa.com au press@betpawa.com

Kuhusu betPawa

betPawa ni chapa ya michezo ya kubashiri, inayomilikiwa na Mchezo Limited yenye makao makuu nchini Rwanda. betPawa inafanya kazi katika nchi 11 barani Afrika, ikiwa na watumiaji

zaidi ya milioni 10. betPawa ina dhamira ya kufanya michezo ya kubahatisha kuwa rahisi, kwa kutoa usaidizi kwa wateja wa masaa 24, jukwaa linalofaa mtumiaji, kiwango cha chini zaidi cha kubashiri na malipo ya uhakika.

Send this to a friend