Wateja wa TotalEnergies kurudishiwa 10% kupitia ushirikiano na LIPA KWA M-PESA

0
55

Dar es Salaam – Juni 21, 2023. Kupitia dhamira ya kuendeleza mfumo wa
maisha wa kutotumia pesa taslimu nchini, huduma ya M-Pesa ya Vodacom na
TotalEnergies Marketing Tanzania Limited wamezindua ushirikiano wa
kimkakati ili kuwawezesha wateja kufanya malipo bila ya kutumia pesa taslimu
kwa usalama na urahisi katika vituo vyote vya kutolea huduma vya
TotalEnergies.

Kupitia ushirikiano huu mpya, wateja watafurahia faida tofauti ikiwemo
kurudishiwa 10% ya pesa watakapolipia kwa kutumia M-Pesa kwa siku 15
zijazo. Ofa hii itaendelea mbele zaidi kwa kila Jumamosi kwa miezi mitatu
ijayo. Zaidi ya hapo, kupitia ushirikiano huu, pia wateja watapata huduma ya
M-Pesa kwa shughuli za kibiashara ikiwamo kuweka, kutoa, na kutuma pesa
wakiwa katika katika vituo vya kutolea huduma vya TotalEnergies.

Ushirikiano wa TotalEnergies na huduma ya M-Pesa ya Vodacom umekuja
katika muda muafaka, sio kuwapa Watanzania njia rahisi na ya uhakika ya
kutumia pesa bali pia kuunga mkono jitihada za kidigitali za serikali hususani
kuchochea mabadiliko kuelekea kwenye uchumi wa kidigitali ambapo bado
matumizi ya pesa taslimu yanaendelea kutumika na kukubalika maeneo
mengi nchini kote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huu uliofanyika katika kituo
cha kutolea huduma cha TotalEnergies kilichopo Oysterbay jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania PLC, Bi.
Harriet Lwakatare amesisitiza namna ambavyo kampuni hiyo imekuwa mstari
wa mbele kwenye kuunga mkono ajenda ya Tanzania ya kidigitali na kuwa
ushirikiano huu mpya ni hatua mojawapo kuelekea njia sahihi.

“Tunaendelea kujikita katika kutoa ubunifu wa ufumbuzi wa kidigitali
kuhakikisha tunasaidia mamilioni ya Watanzania kujiunga na kushiriki katika
uchumi wa kidigitali. hili linathibitishwa kwa ubunifu tunaoendelea kuufanya
katika kuunga mkono ajenda ya kutotumia pesa taslimu ambapo M-Pesa ina
mchango muhimu ambapo tumeleta mapinduzi ya namna tunavyofanya
malipo. Ushirikiano huu utasaidia wateja wa TotalEnergies kulipia kwa urahisi
kupitia M-Pesa kwa kufuata hatua chache kwenye simu zao za mkononi na
kupata huduma mbalimbali kwa urahisi na usalama wa miamala yao wakiwa
katika vituo vya kutolea huduma vya TotalEnergies,” alisema Bi. Lwakatare.

Kwa upande wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Meneja Masoko,
Caroline Kakwezi ameelezea kuwa, “TotalEnergies imevutiwa na jitihada za
Vodacom kuunga mkono kasi ya utekelezaji wa dhamira ya serikali ya kutumia
mifumo ya kidigitali kwenye kuleta uchumi jumuishi Tanzania kupitia M-Pesa.
Ushirikiano huu kati ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited na huduma
ya M-Pesa ya Vodacom unaendelea kuchochea zaidi juhudi hizi kwa
kuwawezesha wateja kulipia mafuta kupitia Lipa Kwa Simu na kupata huduma za M-Pesa za kuweka na kutoa pesa.

Ushirikiano huu mpya unalenga kuwajengea hali ya kujiamini katika matumizi ya majukwaa ya kifedha ya kidigitali kwa kupunguza hatari na mzigo unaosababishwa na kutembea na
pesa taslimu. Kwa pamoja, Vodacom na TotalEnergies tutaendelea kujizatiti
kutoa huduma bora kwa wateja.”

Miaka 10 iliyopita na zaidi, Tanzania imeshuhudia mwamko mkubwa wa
matumizi ya huduma za pesa kwa njia ya simu za mkononi kama vile M-Pesa
ambayo inaoongoza njia kwa upande wa malipo ya kidigitali. ikiwa na wateja
zaidi ya milioni 10 na wafanyabiashara zaidi ya 180,000 kwenye mtandao
wake wakitoa huduma ya LIPA KWA M-Pesa na suluhisho kwa huduma za
wafanyabiashara, M-Pesa inaendelea kuwa kinara kupitia ubunifu wa
ufumbuzi wa malipo ya kidigitali ambayo yanaleta urahisi, ufanisi na hatimaye
kuchochea ujumuishi wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote.

Kwa kuongezea, kampuni hizi mbili zinaamini kuwa safari ya kuelekea katika
uchumi usiotegemea matumizi ya pesa taslimu ni suala ambalo linaweza
kufikiwa na ni hatua muhimu kwenye uchumi wa Tanzania na zinatumaini
kuwa ushirikiano huu utakuwa na mchango chanya kwa Maisha ya
Watanzania.

Send this to a friend