Tigo yaingiza sokoni ‘Kitochi 4G Smart’ ’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu
Dar es Salaam. Oktoba 31, 2019. Kampuni inayoongoza katika mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo, leo imezindua simu yenye sifa zasmartphone ‘‘Kitochi 4G Smart’ ya kwanza kwenye soko la simu Tanzania yenye uwezo wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote ili kufungua fursa za kijamii na kiuchumi.
Simu hiyo inayojulikana kama ‘Kitochi 4G Smart’ inapatikana sokoni kwa gharama nafuu ya Sh49, 000/- na inakuja na Applications kama WhatsApp, Facebook, Twitter na YouTube.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema “Kama waanzilishi wa kwanza wa mtandao wa kasi wa 4G hapa nchini tangu mwaka 2014, tunavunja mipaka tena kwa kuhakikisha kila mmoja anapata simu ya 4G kwa gharama nafuu ili kuwa sehemu ya mabadiliko ya kidigitali na hatimaye kuchangia ujumuishwaji wa kidigitali hapa nchini,” alisema Boudiaf.
Boudiaf aliongeza kuwa kwa muda mrefu gharama kubwa ya simu zenye uwezo wa 4G imekuwa kikwazo kwa watanzania wengi kumiliki simu zenye uwezo wa intaneti ya kasi hivyo ujio wa simu hiyo ni msaada kwa watanzania wengi.
“Kwa ujio wa simu hii ya ‘Kitochi 4G Smart’ kwenye soko yenye uwezo wa Facebook ya bure kwa miezi mitatu itawapa wateja wetu uwezo wa kujumuika kwenye mitandao na hivyo kufanya kila mmoja kuwa sehemu ya mageuzi ya kidigitali,” alisema.
Naye, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema “Kitochi 4G Smart inadhihirisha dhamira ya Tigo ya kuwahudumia wateja wake katika kila hatua ya maisha.Kwa hatua hii ni imani yetu kuwa hakuna mtu ambaye atashindwa kupata manufaa yatokanayo na intaneti ya kasi ya 4G.”
Aliongeza, “Kitochi 4G Smart itaongeza wigo wa upatikanaji wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote na kusaidia katika ufikiwaji wa taarifa na maarifa yatakayosaidia katika kutumia vema fursa za kijamii na kiuchumi.”
Tigo inapanua wigo wa uvumbuzi kwa kuendelea kutoa bidhaa na huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja sokoni na zaidi kuchangia mageuzi ya kidigitali nchini.Kitochi 4G Smart ni hatua nyingine kutoka Tigo baada ya Smartphone ya Kiswahili, Facebook ya bure, App ya Tigo Pesa Pesa na App ya Tigo.
Wateja wa Tigo wanaweza kujipatia simu ya Kitochi 4G kwa kuweka oda kwa kupiga namba 100 na kufanya malipo ya awali.
Kitochi 4G Smartinakuja na App kama Facebook, WhatsApp, YouTube,Twitter, Gmail, Google Map na zingine nyingi zinazopatikana kwenye kaiOS App store.