
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa jumla ya watia nia 5,475 wamechukua fomu za kuwania kugombea ubunge kupitia chama hicho, ambapo kati yao, 4,109 wanawania katika majimbo ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, kati 4,109 ya waliochukua fomu katika majimbo ya uchaguzi, 3,585 ni kutoka Tanzania Bara huku 524 wakitoka Zanzibar.
Huu ni sawa na wastani wa watia nia 15 katika kila jimbo la uchaguzi, kwenye majimbo yote 272 nchini.
Aidha, Makalla amevitaka vikao vya uchujaji wa wagombea kutenda haki katika mchakato wa kuchuja wagombea baaada ya zoezi la uchukuaji wa fomu.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeingiza TZS bilioni 2.7 kutokana na ada ya fomu za kuwania kugombea ubunge. Fomu moja ya ubunge ni TZS 500,000, ambapo jumla ya wanachama 5,475 wamechukua fomu.







