Watoto 18 wafariki baada ya kunywa dawa yenye ‘sumu’  

0
55

Takriban watoto 18 wamefariki dunia nchini Uzbekistan baada ya kunywa dawa iliyotengenezwa na mtengenezaji wa dawa wa India Marion Biotech, kulingana na Wizara ya Afya ya Uzbekistan.

Wizara hiyo imesema watoto 18 kati ya 21 waliokuwa na ugonjwa wa kupumua waliotumia syrup ya Doc-1 Max papo hapo walipoteza maisha baada ya kuinywa.

Katika taarifa iliyotolewa na wizara Jumanne Desemba 27, 2022 ilisema kundi la syrup lilikuwa na ethylene glikoli, ambayo ni dutu yenye sumu. Dawa hiyo iliingizwa nchini Uzbekistan na Quramax Medical huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Lowasa alazwa Afrika Kusini kwa matibabu

Pia ilisema syrup hiyo ilitolewa kwa watoto majumbani bila agizo la daktari, au kwa ushauri wa wafamasia, na kufanya kipimo kilichozidi kiwango cha kawaida cha watoto. Haijabainika mara moja ikiwa watoto wote walikuwa wametumia zaidi ya kiwango cha kawaida.

Tukio la Uzbekistan linafuatia kama lile lililotokea huko nchini Gambia, ambapo vifo vya watoto wasiopungua 70 vilisababishwa dawa ya kikohozi zilizotengenezwa na Maiden Pharmaceuticals yenye makao yake New Delhi. Serikali ya India na kampuni zote mbili zimekanusha kuwa dawa hizo zilikuwa na makosa.

Send this to a friend