Watoto wafariki kwa kutumbukia kisimani wakicheza

0
41

Watoto wawili, mmoja wa miaka 3 na mwingine wa mwaka mmoja na nusu wakazi wa Nyantorontoro B Halmashauri ya Mji Geita mkoani Geita wamefariki dunia kwa kutumbukia kisimani wakati wakicheza.

Mwakilishi wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Geita, Emmanuel Ndoji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa watoto hao wametumbukia kwenye kisima hicho wakiwa wanacheza peke yao.

Mwenyekiti UVCCM auawa baada ya kufumaniwa

Amesema chanzo cha tukio hilo uzembe wa wazazi wao baada ya kuwaacha watoto hao peke yao hali iliyosababisha kwenda kwenye bwawa hilo kuchota maji na kusababisha vifo vyao.

Aidha, Jeshi hilo limewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuacha kutelekeza watoto katika mazingira hatarishi hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

Send this to a friend