Watoto wamuua mama yao wakidai anaroga wajukuu

0
48

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya mama yao mzazi, Shija Mageranya (77) mkazi wa Kijiji cha Ndua, Kata ya Kasororo wilayani Misungwi wakimtuhumu kuwa ni mshirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema mauaji hayo yametokea Juni mosi, 2024 katika kijiji hicho ambapo watoto hao walikuwa wakimtuhumu mama yao kuwa anawaroga wajukuu zake na kusababisha wapate wendawazimu na hata vifo visivyoeleweka.

Ameeleza kuwa majira ya saa 2:30 usiku wakati Bibi huyo akipata chakula cha usiku pamoja na wajukuu wake, ghafla waliingiliwa na mwanaume ambaye aliwasalimia kisha akachomoa panga lenye ncha kali na kuanza kumshambulia bibi huyo kwa kumkata sehemu za kichwani na mabegani.

Mke ashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mume wake akishirikiana na hawara

“Kufuatia tukio hilo, Bibi huyo alivuja damu nyingi hadi kupelekea kupoteza maisha, na baada ya tukio hilo mwanaume huyo ambaye hakuweza kutambulika kwa wakati huo, alikimbia na kuwaacha watoto wale wakiwa wamesambaa huku wakimshuhudia bibi yao akikata roho mbele yao,” amesema.

Watuhumiwa hao wanaoshikiliwa ni Kashinja Dotto (55), Joseph Dotto (20), Magerani Dotto (44), Nyanzala Dotto (34), Masaga Dotto (46) na Milapa Dotto (30) ambao walipanga njama kwa kushirikiana na watu wengine ambao bado wanatafutwa.

Send this to a friend