Watoto wanne wa familia moja wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa kwa moto uliodaiwa kuwashwa na mganga wa kienyeji kwa lengo la kuondoa mikosi katika familia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tayari mganga huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Diwani wa Kata ya Kigwa, Bakari Kabata amesema mmiliki wa mji huo alimuita mganga kwa lengo la kumuondolea mikosi kwenye nyumba yake, na wafamilia wapatao ishirini walikuwa kwenye kibanda kilichowashwa moto na mganga huyo aliyewapa sharti la kutoka mmoja mmoja baada ya moto huo kuwashwa.
Ajikuta ndani ya jeneza amezikwa futi sita baada ya kulewa kupita kiasi
Ameeleza kuwa baada ya moto kuwa mkali, ulisababisha wanafamilia kusukumana kutoka nje ili kujiokoa, na ndipo watoto hao wanaokadiriwa kuwa na umri usiozidi miaka kumi na tano kukutwa na umauti.
Kwa mujibu wa Diwani huyo, mama wa familia ni miongoni mwa majeruhi saba waliolazwa hospitali ya Omulinga na hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete.