Watoto watano wafariki kwa ugonjwa usiojulikana Arusha

0
43

Watoto watano wa familia moja wakazi wa kijiji cha Mswakini wilayani Monduli, mkoa wa Arusha, wamefariki dunia kwa ugonjwa ambao bado haujatambulika baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo na tumbo kujaa.

Diwani wa Kijiji cha Mswakini, Nanga Lenasira Mollel amesema vifo vya watoto hao vimetokea kwa nyakati tofauti kuanzia Julai 5 hadi leo Julai 19 ambapo amefariki mtoto mwingine aliyekuwa amebakia katika hospitali ya Mount Meru Arusha.

Amesema mtoto wa kwanza, Bosi Nyangusi alifariki Julai 5, 2022 kutokana na kusumbuliwa na tumbo, na baadaye wanzake wanne walipelekwa hospitali ya TMA Monduli kwa ajili ya matibabu kisha wakaruhusiwa. Wakati wakiwa njiani walizidiwa na kupelekwa Mout Meru, ambapo Julai 16 alifariki Saimalie.

Ameongeza kuwa, baadaye watoto wawili walifariki Julai 17 ambao ni Lemali na Sophia, huku aliyekuwa amebaki amelazwa hospitali ya Mount Meru, Veronica aliyekuwa anasoma darasa la tatu Mswakini kufariki leo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mswakini, Nanga Karani amesema wamekuwa wakifuatilia chanzo cha vifo hivyo bila mafanikio.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend