Watoto wateketea kwa moto wakati wazazi wakiwa kwenye maombi ya usiku

0
64

Kijiji cha Ramula, katika eneo la Gwassi Magharibi, Kaunti Ndogo ya Suba Kusini nchini Kenya kimekumbwa na huzuni na simanzi baada ya watoto wawili wa familia moja kufariki dunia kwa kuteketea kwenye moto ulioshukiwa kuwa wa kuchomwa makusudi.

Watoto hao, waliotambulika kama Saviour Omondi, mwenye umri wa miaka mitatu na mwanafunzi wa chekechea (PP1) katika Shule ya Msingi Ramula, pamoja na kaka yake Reagan Otieno, walikuwa wamelala wakati nyumba yao iliposhika moto mwendo wa saa 9 alfajiri Jumamosi.

Moto huo ulioteketeza nyumba yao uliwaacha watoto hao wakiwa wameungua vibaya kiasi cha kutotambulika.

Chifu wa eneo hilo, Tobias Opiyo amesema tukio hilo lilitokea wakati wazazi wa watoto hao walipokuwa wameenda kwenye ibada ya maombi ya usiku katika nyumba ya jirani ambapo baba yao alifika baada ya kusikia mayowe kutoka kwa mke wake wa kwanza aliyekuwa amelala katika moja ya nyumba hizo.

Send this to a friend