Watu 10 wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Tanga

0
71

Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imewahukumu watu 10 adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji ya aliyekuwa mlinzi wa ofisi ya kijiji cha Lulago wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Mbwana Salim Kilo yaliyofanyika Oktoba 10, 2013.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Mfawidhi Kanda ya Tanga, Latipha Mansoor amesema kutokana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili, Mahakama imejiridhisha na kuwatia hatiani watuhumiwa.

Awali washtakiwa hao walikua 20 ambapo walishtakiwa kwa kosa la ugaidi huku tisa kati yao wakiachiwa huru baada ya Mahakama kukosa ushahidi mwaka 2022 na baadae mashtaka yakabadilishwa na kuwa kesi ya mauaji.

Asilimia 82 ya madereva Kenya wafeli mtihani wa udereva

Waliohukumiwa ni Haji Omary Mzana, Khalid Salehe Sekinzu, Omary Said, Toba Salehe Sekinzu, Abdallah Mrisho, Mnyamisi Said, Abdulrahman Hassan, Juma Omary, Ramadhani Athuman Mnguu na Jawa Omari Mzana huku mshtakiwa mmoja akiachiwa huru baada ya upande wa ushahidi kuonyesha kuwa ameshtakiwa kwa jina lisilokuwa la kwake.

Send this to a friend