Watu 11 wa ‘Tuma kwa namba hii’ wahukumiwa jela miaka mitatu

0
38

Watu 11 wakazi wa Ifakara mkoani Morogoro wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni 6 kwa kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kutoa taarifa za uongo mtandaoni.

Hukumu hiyo imetolewa Machi 26, mwaka huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Annah Magutu baada ya washtakiwa hao kusomewa na kukiri mashtaka yanayowakabili.

Watu 12 wakamatwa Zanzibar kwa kula hadharani kipindi cha mfungo

Washtakiwa hao ambao ni Fredrick Kanepela, Julius Mwabula, Amiry Luwiso, Tareeq Sadrudin, Ashraf Awadhi, Frank Kifyoga, Samson Tandike, Michael Haule, Mussa Maganga, Helman Lwambano na Kelvin Mkapila ni miongoni mwa washtakiwa 23 wa kesi hiyo.

Wakisomewa mashitaka yao na jopo la mawakili wa Serikali, wameeleza kuwa washtakiwa hao walijipatia fedha kwa kutuma jumbe mbalimbali kwa wananchi unaosema “nitumie hiyo hela kwenye namba hii” pamoja na kupiga simu wakidai wao ni wafanyakazi wa kampuni za simu na kutapeli pesa.

Send this to a friend