Watu 12 wakamatwa Zanzibar kwa kula hadharani kipindi cha mfungo

0
47

Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja linawashikilia watu 12 kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abubakar Ally amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonyesha baadhi ya watu katika eneo la Viwanja vya Mnazi Mmoja wakila hadharani wakati wa mchana.

“Kama mlivyosikia au mlivyoona juzi juzi kulikuwa na watu walisemekana pale Mnazi Mmoja wanafanya uhalifu na kula hadharani, basi siku ya pili yake tulifanya oparesheni kali ya msako na watu hawa walikamatwa maeneo ya Mnazi Mmoja kama ambavyo ile ‘clip’ ilikuwa ikisema, na tulikamata takribani watu 12 tunao mpaka sasa hivi hapa na vielelezo vyao,” ameeleza Kamanda.

Aidha, Kamanda Ally amesema jeshi hilo linaendelea kukamilisha taratibu za kiupelelezi ili watuhumiwa hao waweze kufikishwa mahakamani.

Send this to a friend