Watu 12 wamefariki katika ajali Dodoma

0
37

Watu 12 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Frester lililokuwa likitoka Bukoba kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na Lori lenye shehena ya saruji.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kumkia leo Februari 9, 2023 saa sita usiku katika Kijiji Cha Silwa Pandambili barabara kuu ya Dodoma – Morogoro huku chanzo cha ajali hiyo kikidaiwa ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Awadh Haji amefika eneo la ajali na kutoa rai kwa madereva kuzingatia usalama na sheria za barabarani.

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni siku chache tangu kutokea kwa ajali nyingine wilayani Korogwe mkoani Tanga iliyohusisha gari ya mizigo ‘Fuso’ na Coaster na kupelekea vifo vya watu 20 wakiwemo watu 14 wa familia moja waliokuwa wakisafirisha mwili wa marehemu kwenda kuzika mkoani Kilimanjaro.

Send this to a friend