
Shirika la Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC) limethibitisha ongezeko la visa 12 vya ugonjwa wa Ebola katika mikoa miwili tofauti nchini Uganda
Tangu kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwezi Januari mwaka huu, Uganda imerekodi visa 14 na vifo viwili vitokanavyo na Ebola ambapo watu wawili akiwemo msichana wa miaka minne na muuguzi wamepoteza maisha.
‘’Kuzuka kwa ugonjwa Ebola nchini Uganda ni changamoto kwani visa zaidi vinaendelea kuripotiwa. Hata hivyo nina imani mamlaka husika inafanya kila iwezalo kufuatilia waliotangamana na wagonjwa hao,’’ imesema CDC.
Si mara ya kwanza kwa Uganda kuripoti maambukizi ya Ebola, mwaka wa 2022 watu 55 kati ya 143 waliougua ugonjwa huo walifariki na baadaye mwaka 2023 maambukizi ya ugonjwa huo yalitangazwa kuisha.