Watu 14 wafariki, 22 wajeruhiwa ajalini mkoani Mtwara

0
14

Watu 14 wameofariki dunia na wengine 22 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea Januari 2, 2022, saa 2:15 usiku katika Kijiji cha Lidumbe, Wilaya ya Newala mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara ACP Mark Njera chanzo cha ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya ‘Uchumi’ Mtwara-Tandahimba-Newala-Masasi ni mwendokasi wa dereva wa gari aina ya Scania wakati aliposhindwa kulimudu na kwenda kuwagonga watu hao.

Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

Rais Samia amemtaka Brigedia Jenerali Gaguti kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa, marafiki na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Aidha, amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama wa barabarani kuongeza juhudi za kudhibiti ajali hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka, na pia amewaasa madereva kufuata na kuzingatia Sheria za usalama barabarani.

Send this to a friend