Watu 17 wafariki ajalini Tanga wakisafirisha maiti

0
49

Watu 17 wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa  katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Magira Gereza wilayani Korogwe mkoani Tanga majira ya saa 4:30 usiku Februari 3, 2023.

Mkuu wa Mkoa Wa Tanga, Omary Mgumba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha gari aina ya Fuso na Coaster iliyokuwa na watu 26 ikisafirisha mwili wa marehemu kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro.

Miili hiyo imehifadhiwa katika Hospitali  ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo, huku majeruhi wawili wakibaki Hospitali ya Wilaya, Magunga, Korogwe.

Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa Fuso ambapo alijaribu kulipita gari la mbele bila kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso gari coaster hiyo.

Send this to a friend